Victor Akpan ni Mnyama

Klabu yetu imefikia makubaliano ya kumsajili kiungo mkabaji Victor Akpan raia wa Nigeria kutoka Coastal Union kwa mkataba wa miaka miwili.

Akpan amekuwa mhimili katika kiungo cha ulinzi cha Coastal akiiwezesha kufika Fainali ya Michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) msimu uliopita.

Akpan amekuwa kwenye kiwango bora ba analijua vizuri soka la Bongo na mazingira yake ndiyo moja ya sababu iliyotufanya tumsajili.

Msimu uliopita Akpan amecheza mechi 26 akifunga bao moja na kusaidia kupatikana kwa mengine manne.

Kabla ya kujiunga na Coastal Union Akpan alikuwa anachezea JKU ya Zanzibar aliyojiunga nayo akitokea Katsina United ya nchini kwao Nigeria.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER