Jezi zetu za Msimu Mpya wa Ligi 2021/22 tayari zimetoka na zipo mtaani zinauzwa katika maduka yote ya Vunjabei nchi nzima kuanzia leo.
Uzinduzi rasmi wa jezi hiyo utafanyika kesho lakini kutokana na uhitaji mkubwa wa mashabiki wetu tumeamua kuzitoa leo ili kukata kiu yao.
Jezi yetu ya msimu huu imekuwa na ubora mkubwa na itauzwa kwa aina tofauti ya bei kulingana na ubora na kipato cha mashabiki wetu.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano, Ezekiel Kamwaga amesema jezi hizo zitaanza kuuzwa kwa bei ya sh 25,000 na kuendelea kulingana na ubora wake.
“Jezi yetu rasmi kwa ajili msimu wa 2021/22 tayari imetoka na inaptiakana kuanzia muda huu kwenye maduka ya Vunjabei nchi nzima na vile vile kupitia Simba App. Tumeamua kuzitoa leo kutokana na maombi ya mashabiki wetu lakini uzinduzi utafanyika kesho,” amesema Kamwaga.