Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Boniface Lihamwike ametangaza rasmi Januari 29, 2023 kuwa ndio itakuwa tarehe ya uchaguzi mkuu wa klabu.
Lihamwike amesema Uchaguzi wa safari hii tutatumia kanuni zetu wenyewe nasi za Shirikisho la soka Tanzania (TFF) ambazo tulitumia katika chaguzi zilizopita.
Nafasi zitakazogombewa ni Mwenyekiti (nafasi moja), Mjumbe wa Bodi (nafasi moja) na Wajumbe wa Bodi (Nafasi nne).
Mwenyekiti atakayechaguliwa atakuwa na nafasi ya kuchagua wajumbe wawili na kufanya kufika nane kwa mujibu wa kanuni.
Zoezi la kuchukua na kurudisha fomu litaanza rasmi Desemba 5 hadi 19 katika ofisi za klabu zilizopo Masaki Jijini Dar Es Salaam.
Vigezo vya Wagombea
– Mwadilifu, mwaminifu
– Mwanachama hai wa klabu
– Shahada ya Chuo Kikuu (Mwenyekiti) na Mjumbe mmoja wa Bodi.
– Mjumbe wa Bodi awe na cheti cha Sekondari.
– Uzoefu wa angalau miaka mitatu wa kuongoza soka.
– Asiwe amepatikana na hatia ya kosa la jinai na kuhukumiwa.
– Awe angalau na umri wa miaka 25 na isizidi miaka 64.
– Asiwe mwanahisa au mmiliki wa klabu nyingine ya soka.
– Asiwe mwamuzi wa soka.
Ratiba Kamili ya Uchaguzi
– Disemba 5-19 kuchukua na kurejesha fomu
– Disemba 20 Ukaguzi wa fomu zilizorudishwa ndani ya muda.
– Disemba 22-24 Usaili wa watia nia waliorudisha fomu kwa wakati.
– Disemba 28 kubandika majina ya wagombea waliopitishwa.
– Disemba 29 Kupokea mapingamizi dhidi ya Wagombea.
– Januari 1-2 Kupitia mapingamizi.
– Januari 3-4 kusikiliza na kutoa uamuzi wa mapingamizi.
– Januari 5 kutangazwa majina ya wagombea waliokidhi vigezo.
– Januari 6-28 Kampeni
– Januari 29 Uchaguzi.