Tutakutana na Al Ahly Tripoli Kombe la Shirikisho Afrika

Kati ya Septemba 13 hadi 15 tutacheza mchezo wetu wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya kwanza dhidi ya Al Ahly Tripoli kutoka Libya.

Mchezo huo utakuwa wa ugenini ambao utapigwa nchini Libya kabla ya mechi ya marudiano ambayo itapigwa jijini Dar es Salaam, kati ya Septemba 20 hadi 22.

Al Ahly Tripoli imefika hatua hiyo baada ya kuitoa Uhamiaji kutoka Zanzibar kwa jumla ya mabao 5-1.

Sisi ni miongoni mwa timu chache zenye pointi nyingi Afrika ambazo hazikuanzia hatua ya awali.

Mshindi wa jumla kati yetu na Al Ahly Tripoli ataingia moja kwa moja katika hatua ya makundi ya michuano hiyo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER