Tutaanza Kutangaza Utalii wa Zanzibar

Leo tumetangaza kuanza kutangaza vivutio vya Utalii wa Zanzibar kupitia kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea.

Mtendaji Mkuu wa Klabu, Imani Kajula amesema kama tulivyofanya mwaka jana kutangaza Utalii wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika sasa tumehamia Zanzibar.

Kajula amesema kuanzia katika mchezo wa kesho dhidi ya Singida Big Stars jezi zetu zitaandikwa Visit Zanzibar kwenye mabega.

“Tulianza Bara sasa tumekuja Zanzibar na kutangaza Utalii. Simba ni kubwa na ina wafuasi wengi kwenye mitandao ya kijamii kwahiyo kupitia michuano hii tutasaidia kukuza uchumi,” amesema Kajula.

Aidha Kajula amesema mara zote Simba imekuwa ikishirikiana na Serikali katika mambo mbalimbali ikiwemo suala la Utalii

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER