Tupo tayari kwa Namungo

Kikosi chetu leo kitashuka katika Uwanja wa Amani kucheza mechi ya Nusu Fainali ya Michuano ya Mapinduzi dhidi ya Namungo utakaopigwa saa 2:15 usiku.

Kama tulivyoahidi kabla ya kwenda kwenye michuano hiyo kuwa lengo letu ni kuhakikisha tunatwaa ubingwa wa michuano hii na hakuna kilichobadilika.

Maandalizi ya mchezo yamekamilika wachezaji wapo katika hali nzuri hakuna tutakayemkosa kwa sababu za majeruhi.

KAULI YA KOCHA PABLO

Kocha Mkuu Pablo Franco, amesema mchezo utakuwa mzuri kutokana na aina ya uchezaji wa Namungo kuwa si wa rafu kama mechi zilizopita.

“Mchezo utakuwa mgumu, Namungo ni moja ya timu nzuri. Tunaamini itakuwa mechi bora ya kutazama kwa kuwa timu zote zinacheza soka na si vurugu,” amesema Pablo.

SAFARI YETU KATIKA MICHUANO HII

Katika michuano hii ya Mapinduzi tulipangwa Kundi C pamoja na timu za Selem View na Mlandege. Tulimaliza vinara kwa kushinda mechi moja na kutoka sare moja.

Matokeo yalivyokuwa

Simba 2-0 Selem View
Simba 0-0 Mlandege

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER