Tupo tayari kwa mchezo dhidi ya Namungo

Tupo tayari kwa mchezo dhidi ya Namungo

Kikosi chetu leo saa 10:15 jioni kitashuka katika Uwanja wa KMC Complex kuikabili Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Tutaingia kwenye mchezo wa leo tukiwa na kumbukumbu ya ushindi wa bao moja tuliopata ugenini dhidi ya Tanzania Prisons siku mbili zilizopita.

Tunatarajia kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Namungo lakini malengo yetu ni kuhakikisha tunashinda na kupata alama tatu muhimu nyumbani.

Kocha Wilken afunguka…..

Kocha Msaidizi, Darian Wilken amesema mchezo wa kesho wa leo utakuwa mgumu lakini tumejipanga kuhakikisha tunapata ushindi kwenye uwanja wa nyumbani.

Kocha Wilken amesema Namungo ni timu nzuri hasa ikichangiwa na kuwa na Kocha mpya ambaye amewaongezea morali wachezaji wake lakini itakutana na wapinzani bora zaidi yako.

“Utakuwa mchezo mgumu, Namungo ni timu imara yenye wachezaji wazoefu na tayari imepata kocha mpya, lakini Simba ni kubwa zaidi na ipo tayari kupambana hadi mwisho kwa ajili ya kupata pointi tatu,” amesema Kocha Wilken.

Wachezaji wanaitaka mechi……

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji mlinda mlango, Ally Salim amesema kwa upande wao wapo tayari kupambana hadi mwisho kwa ajili ya kupata pointi tatu.

Ally amesema Namungo ina wachezaji wengi wazoefu ambao wengi walikuwa nao lakini Simba ni kubwa na pamoja na changamoto zote ila tupo tayari kwa ajili ya pointi tatu muhimu za nyumbani.

“Sisi tupo tayari kwa mchezo, Namungo tunawaheshimu ni timu bora lakini Simba ni bora zaidi na tupo kwa ajili ya kupigania alama tatu,” amesema Ally Salim.

Hali ya kikosi….

Kikosi kipo kwenye hali nzuri wachezaji wote walioshiriki mchezo dhidi ya ya Tanzania Prisons wapo tayari kwa ajili ya mechi ya leo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER