Tupo tayari kwa Dabi ya Kariakoo

Leo saa 11 jioni kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Yanga katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu ya NBC.

Mchezo wa leo ni muhimu kushinda kwakuwa utaamua ubingwa wa msimu kutokana na tofauti ya alama moja iliyopo baina yetu.

Mara zote mechi ya Dabi Kariakoo imekuwa ngumu na haina mwenyewe lakini tumejipanga na tupo tayari kwa ajili mchezo huo.

Kauli ya Fadlu kuelekea mchezo wa Dabi…

Kocha Mkuu, Fadlu Davids amesema kikosi kipo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo na malengo yetu ni kuhakikisha tunashinda.

Fadlu ameongeza kuwa tunategemea utakuwa mchezo mgumu kutokana na ubora wa wapinzani hasa ukizingatia ni mechi ya kuamua ubingwa wa msimu.

“Kikosi chetu kipo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo. Hii ni Dabi na mara zote inakuwa na upinzani mkubwa lakini tupo kamili kuhakikisha tunapata ushindi,” amesema Fadlu.

Dabi ya kwanza ya Kariakoo kwa Mpanzu

Kiungo mshambuliaji, Elie Mpanzu leo atacheza mechi yake ya kwanza ya Dabi ya Kariakoo.

Mpanzu amejiunga nasi kwenye dirisha dogo la usajili la mwezi Disemba kwahiyo leo itakuwa ni mara yake ya kwanza kukutana na presha ya Dabi ya Kariakoo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER