Tupo tayari kumalizia kazi tuliyoianza Zanzibar

Leo saa 10 jioni kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa Moses Mabhida kuikabili Stellenbosch katika mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Tutaingia katika mchezo wa leo tukiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa bao moja tuliopata kwenye mechi ya mkondo wa kwanza iliyopigwa katika Uwanja wa Amaan Zanzibar, Aprili 20.

Lengo letu ni moja tu kwenye mchezo wa leo kuhakikisha tunapambana hadi mwisho kuhakikisha tunafanikiwa kitinga fainali.

Kocha Fadlu awasisitiza wachezaji kuhusu umakini

Kocha mkuu, Fadlu Davids amewasisitiza wachezaji kuwa makini muda wote kuhakikisha hatufanyi makosa ambayo yatapelekea kuruhusu bao.

Fadlu amesema anafahamu Stellenbosch itakuja kwa nguvu ya kutaka kutapata bao la mapema lakini tayari tumejipanga kwa hilo huku pia akiwaambia wachezaji kuwa watulivu katika kutumia nafasi tutakazopata.

“Tuna kibarua kigumu lakini malengo yetu ni kuhakikisha tunavuka na kutinga fainali. Tunahitaji sare ya aina yoyote kama ikishindikana kabisa hata bila kufungana lakini tumejipanga kutafuta bao la ugenini ili kuwapa wakati mgumu wapinzani,” amesema Fadlu.

Mukwala asema kazi bado haijaisha

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji mshambuliaji, Steven Mukwala amesema katika mchezo wa mkondo wa kwanza tuliibuka na ushindi wa bao moja kule Zanzibar na tunahitaji kuulinda ili kupata nafasi ya kutinga fainali.

“Bado kuna dakika 90 za kupambana ili kufikia malengo yetu tuliyojiwekea. Bao moja tuliloshinda nyumbani hatuwezi kusema limetuvusha moja kwa moja tupo tayari kupambana hadi mwisho kuona tunaweza kufika fainali,” amesema Mukwala.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER