Tupo Sokoine leo kupigania alama tatu

Leo saa 10 jioni kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya kuikabili Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Mchezo wa leo utakuwa ni wa nne w ligi ambapo mechi tatu za mwanzo tumefanikiwa kuibuka na alama zote.

Tutaingia kwenye mchezo wa leo tukiwa tunafahamu utakuwa mgumu na tumejipanga kuhakikisha tunafanya jitihada zote uwanjani kuhakikisha tunapata matokeo chanya.

Uwanja wa Sokoine haujawahi kuwa rahisi kwetu kupata alama tatu hasa tunapocheza na Prisons lakini sasa tumejipanga kulikabili jambo hilo.

Robertinho ataka soka safi, pointi tatu…..

Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ ameweka wazi kuwa malengo ya timu ni kushinda mchezo wa kesho kwa kuonyesha soka safi.

Robertinho ameongeza kuwa tutaiheshimu Prisons kwakuwa tunaujua ubora wao lakini hatutaki utuzuie mipango yetu ya kucheza soka safi na kupata alama tatu.

“Tunawaheshimu Prisons, tunakumbuka msimu uliopita walitupa mechi ngumu lakini tumejipanga, sisi tutaingia uwanjani kwa lengo la kucheza soka safi na kushinda,” amesema Robertinho.

Wachezaji wapo tayari kwa mchezo….

Mlinda mlango, Hussein Abel amesema kila mchezaji yupo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo ambao tunahitaji alama tatu muhimu.

“Mara zote tunapokutana na Prisons mchezo unakuwa mgumu, lakini tupo tayari kupambana lengo ni kuhakikisha tunapata alama tatu,” amesema Abel.

Mechi ya mwisho tuliwafunga Sokoine……

Katika mchezo wa mwisho tuliocheza katika Uwanja wa Sokoine tuliwafunga Tanzania Prisons bao moja.

Mchezo huo ulikuwa mgumu na wengi walidhani ungemalizika kwa sare lakini kiungo Jonas Mkude alitupatia bao la ushindi dakika ya 89.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER