Msanii wa Bongo Fleva na Mwanasimba mwenzetu, Tundaman ameibua shangwe la Wenye Nchi Beach Party baada ya kufika na kuanza kuimba pamoja na kucheza na mashabiki.
Tundaman amekuwa pamoja nasi kwenye mambo mengi ikiwemo hamasa mbalimbali kuelekea kwenye mechi zetu za Ligi ya Mabingwa.
Baada ya kufika katika Viwanja vya Coco Beach, Tundaman alienda moja kwa moja kwenye gari la matangazo na kuchukua kipaza kushusha burudani.
Muitikio wa Wanasimba ni mkubwa katika Wenye Nchi Beach Party huku wakinunua tiketi kwa wingi pamoja jezi.