Tunawatakia kheri wachezaji wetu kwenye michuano ya AFCON

Nyota wetu wote sita leo usiku watawakilisha mataifa yao katika mechi zao za kwanza za michuano ya AFCON inayofanyika nchini Ivory Coast.

Wachezaji wetu wote mataifa yao matatu yapo katika kundi moja, Kundi F.

Aishi Manula, Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ Mzamiru Yassin na Kibu Denis watawakilisha Tanzania ‘Taifa Stars’ katika mchezo dhidi ya Morocco ambao utaanza saa mbili usiku.

Henock Inonga ataiwakilisha DR Congo katika mchezo dhidi ya Zambia anayochezea kiungo wetu mshambuliaji, Clatous Chama utakaopigwa saa tano usiku.

Simba inawatakia kheri wachezaji wote sita kuwa na mchezo mzuri na kusaidia mataifa yao kufanya vizuri.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER