Tunatoa basi la klabu kwa mashabiki kwenda Zambia

Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu, Ahmed Ally amesema Menejimenti imetoa basi la timu kwa ajili ya mashabiki kwenda Zambia kuiunga mkono timu kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos utakaopigwa Septemba 16, mjini Ndola.

Ahmed amesema kila shabiki atalipa kiasi cha Shilingi 200,000 na anatakiwa kuwa na viambatanisho vyake vya kusafiria kama paspoti na cheti cha homa ya manjano.

Ahmed amesema safari ya basi la mashabiki itaanza Septemba 13 na kufika Ndola siku mbili baadae ambapo litarejea Septemba 17 mechi ikimalizika.

“Menejimenti ya klabu imeamua kutoa basi kwa ajili ya mashabiki kwenda nchini Zambia kuipa sapoti timu katika mchezo wetu dhidi ya Power Dynamos.

“Basi litaondoka jijini Dar es Salaam, Jumatano Septemba 13 na litafika Ndola Zambia Septemba 15 siku moja kabla ya mchezo wenyewe. Kwa wale wanaotaka kuinga mkono timu wanapaswa kulipa nauli mapema kwakuwa mwisho wa kupokea ni Septemba 10,” amesema Ahmed.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER