Kikosi chetu kinaondoka asubuhi hii kuelekea Visiwani Zanzibar tayari kwa Michuano ya Mapinduzi kikiwa na wachezaji kamili na lengo letu ni kushinda na kurejea na taji jijini Dar es Salaam.
Kwa muda wa miaka kadhaa sasa tumeshindwa kuchukua taji la michuano hii hatua iliyotulazimu kujipanga mwaka huu kuhakikisha tunafanya vizuri na hatimaye kulinyakua.
Kocha Mkuu Pablo Franco, amesema tunakwenda kwa ajili ya ushindani lakini pia kuhakikisha tunashinda taji letu la kwanza kwa mwaka 2022.
Pablo ameongeza kuwa atafanya mabadiliko ya mara kwa mara ya kikosi ili kuwalinda wachezaji kwanj tuna majukumu makubwa baada ya mashindano haya.
“Malengo yetu ni kuhakikisha tunatoa ushindani na kutwaa ubingwa. Hatukufanya vizuri kwa zaidi ya miaka mitano iliyopita kwa hiyo tunataka kubadili upepo na kutwaa ubingwa,” amesema Pablo.
Kikosi chetu kitatupa karata yake ya kwanza Jumatano dhidi ya Selem View katika mchezo utakaopigwa Uwanja wa Amani saa 10:15 jioni.
3 Responses
Together We Can
SimbaSC##NguvuMoja
Safi sana.