Tunafunga Msimu wa Ligi 2021/22 Songea

Kikosi chetu leo kitacheza mechi ya mwisho ya kufungia msimu wa Ligi Kuu ya NBC 2021/22 kwa kuikabili Mbeya Kwanza katika mchezo utakaopigwa katikq Uwanja wa Majimaji mjini Songea.

Ni mchezo muhimu wa ugenini ambao lengo letu kuu ni kushinda kwa kuwa tunahitaji kuwapa furaha mashabiki wetu.

HAITAKUWA MECHI RAHISI

Kaimu Kocha Mkuu Seleman Matola, amesema mchezo utakuwa mgumu ingawa matokeo yake hayatakuwa na athari kwa timu zote zote lakini ushindani utakuwa mkubwa.

Matola amesema maandalizi yamekamilika na wachezaji wamefanya mazoezi ya mwisho jana asubuhi na wapo kwenye hali nzuri tayari kwa mtanange huo.

“Mchezo utakuwa mgumu najua Mbeya Kwanza watataka kupata ushindi hata kama tayari wameshuka daraja lakini sisi tunahitaji kushinda ili kuwapa furaha mashabiki wetu.

“Maandalizi yamekamilika, jana asubuhi tumefanya mazoezi ya mwisho na wachezaji wapo kwenye hali nzuri tayari kwa mchezo wa leo. Lengo ni kuhakikisha tunamaliza msimu kwa ushindi,” amesema Matola.

NYONI AWAITA MASHABIKI

Kiraka, Erasto Nyoni ambaye ni mwenyeji wa Songea amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi katika mchezo wa leo ili kutupa sapoti itakayotuwezesha kupata ushindi.

Nyoni amesema anajisikia furaha kucheza katika Uwanja wa Majimaji kwa kuwa ni nyumbani na ndugu na jamaa zake hupenda kwenda kumtazama kila anapokuja kitu ambacho kinamuongezea morali.

“Huku ni nyumbani najisikia furaha kucheza hapa, marafiki na ndugu zangu huja uwanjani kunitazama pia hapa ndipo historia yangu ya soka ilipoanzia,” amesema Nyoni.

TUTAMKOSA KAGERE

Katika wachezaji tuliosafiri nao tutakosa huduma ya mshambuliaji, Medie Kagere ambaye anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER