Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetangaza ratiba kamili ya Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2023/24 ambayo itaanza kutimua vumbi Agosti 15.
Katika ratiba hiyo sisi tutaanzia ugenini Agosti 17 kuikabili Mtibwa Sugar katika mchezo utakaopigwa Uwanja wa Manungu mkoani Morogoro.
Mchezo wetu wa watani wa jadi umepangwa kufanyika Novemba 5 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 11 jioni ambapo sisi tutakuwa wenyeji.
Tunafahamu ligi ya msimu huu itakuwa ngumu kutokana na kila timu kujipanga vilivyo lakini tumejipanga kuhakikisha tunafanya vizuri kila mchezo.