Tumezindua Mtandao Mpya wa Simba Executive Networks

Kwa kushirikiana na Benki ya CRBD leo tumezindua Mtandao Mpya wa Simba Executive Networks ambao lengo lake kubwa ni kukusanya pesa kuendeleza miundombinu ya klabu ukiwemo Uwanja wetu wa Mo Simba Arena.

Mtandao huu utaongozwa na Viongozi waandamizi ambao moja ya kazi zao ni kuhakikisha miradi ya klabu inasimamiwa na kufanyiwa kazi kama kuwekwa taa na majukwaa katika Uwanja wa Mo Simba Arena ili kuweza kutumika kwa mechi za usiku.

Simba Executive Networks itaongozwa na Mwenyekiti wa Abdulaziz Badru huku Mlezi wake akiwa Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mussa Azan Zungu.

Mtendaji Mkuu wa Klabu, Imani Kajula amesema ili kuwa mwanachama wa Mtandao huu anatakiwa kulipia kiasi cha Shilingi milioni moja na laki tano (1,500,000) kwa mwaka ambapo atalipa kwa miezi mitatu, sita au mara moja kwa mkupuo.

Miongoni mwa vitu anavyopata mwanachama wa Simba Executive Networks

πŸ’  Kila mwaka atapata jezi mpya za kila msimu, kupata tiketi za mechi kubwa na kimataifa

πŸ’  Kupata Bima za maisha

πŸ’  Kutumia miradi yetu kama Uwanja wetu wa Simba Mo Arena kucheza mechi za mabonanza na kufurahia.

Mwanachama wa Simba Executive Networks ambaye atakuwa na kadi ya CRDB atakuwa na uwezo wa kupata yafuatayo.

πŸ’  Atapata Premier Lounge kwenye matawi ya CRDB nchini nzima

πŸ’ Uwanja wa Ndege ukiwa unasubiri Ndege kwa ajili ya safari utakuwa unakula na kunywa.

πŸ’  Saa 24 utakuwa unapata sapoti kutoka CRDB

πŸ’  Kupata Huduma ya Rufaa ya Visa ya Kimataifa

πŸ’  Kununua vitu online popote na kama kikiwa kimeharibika au hakijafika utarejeshewa hela yako

πŸ’  Mwenye kadi akifariki anapewa milioni tano, kama na mume/mke nae ni mwanachama pia anapewa milioni tano inakuwa milioni 10.

πŸ’  Kutoa mpaka milioni 15 pesa taslimu kwa siku kwenye ATM

Pia kutakuwa na akaunti za watoto ambao mtoto anakuwa na visa yaje

Mtoto mwenye akaunti ya Simba Executive Networks akifariki mzazi atapewa milioni mbili.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER