Tumezindua jezi zetu za msimu wa 2024/25 Mikumi

Leo tumezindua jezi kwa tutakazotumia katika msimu mpya wa mashindano 2024/25 ambao utaanza mapema mwezi ujao.

Uzinduzi wa jezi hizo bora na za kisasa zimefanywa na Mtendaji Mkuu wa Klabu Imani Kajula, Mzee Hassan Dalali na Meneja Habari na Mawasiliano Ahmed Ally katika Mbuga za Wanyama Mikumi.

Kama kawaida na utaratibu wetu jezi ya nyumbani itakuwa ni nyekundu, ugenini nyeupe na jezi namba ni bluu.

Baada ya uzinduzi wa jezi hizo kukamilika tayari zimeanza kuuzwa kwenye maduka yote ya Sandaland The Only One nchi nzima.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER