Klabu yetu imezindua jezi maalum ambazo tutazitumia kwenye michuano ya African Football League (AFL) ambayo itaanza Oktoba 20 kwa kucheza na Al Ahly ya Misri.
Jezi hizo ni za aina mbili ambapo ni nyekundu kwa ajili ya mechi za nyumbani na nyeupe kwa ugenini ambazo gharama yake ni Shilingi 35,000 jumla na Shilingi 45,000 rejareja.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu, Salim Abdallah ‘Try Again’ amesema jezi tuliyozindua imetengenezwa kwa kiwango cha juu na inaendana na thamani ya Simba.
Try Again amesema baada ya kukamilika zoezi la uzinduzi jezi zitakuwa tayari zimeanzwa kuuzwa kwenye maduka ya watengenezaji na wasambazi wetu Sandland the Only One.
Try Again amewataka Wanasimba kuhakikisha wananunua jezi hizo kwa wingi ili wageni mbalimbali watakapokuja nchini waone ukubwa wa Simba.
“Katika michuano ya African Football watakuja wageni wengi kwahiyo nawaomba Wanasimba mnunue jezi hizi kwa wingi ili kila watakapopita mitaani waione Simba,” amesema Try Again.
Mtendaji Mkuu wa Klabu, Imani Kajula amesema Simba tuna bahati ya kushiriki michuano hii hivyo kila Mwanasimba anapaswa kuwepo uwanjani Oktoba 20.
Nae Mwenyekiti wa klabu, Murtaza Mangungu amesema kwa wale wanaoleta propaganda kuhusu maandalizi ya timu yetu kuelekea michuano hii hatutaweza kuwaacha na kutotoa kwenye reli badala yake tutapambana nao.