Tumewafunga Stellenbosch Amaan Zanzibar

Mchezo wetu wa kwanza wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Stellenbosch ya Afrika Kusini uliopigwa Uwanja wa Amaan Zanzibar umemalizika kwa ushindi wa bao moja.

Tulianza mchezo kwa kasi huku tulitengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini umaliziaji haukuwa mzuri huku Stellenbosch wakitumia muda mwingi kujilinda na kafanya mashambulizi ya kushtukiza.

Jean Charles Ahoua alitupatia bao hilo pekee dakika ya 45 baada ya kupiga mpira wa adhabu uliotinga wavuni moja kwa moja na kuwashinda walinzi wa Stellenbosch.

Kipindi cha pili hatukurudi kwa kasi kama ilivyokuwa cha kwanza huku Stellenbosch nao wakipata nafasi ya kufika langoni kwetu ingawa tulikuwa imara kuwadhibiti.

Ahoua alipoteza nafasi nzuri ya kutupatia bao la pili dakika ya mwisho ya mchezo baada ya kumpiga hadi chenga mlinda mlango Oscarine kufuatia pasi safi ya Mpanzu lakini mpira aliopiga ulitoka nje kidogo ya lango.

Mchezo wa marudiano utapigwa Jumapili ijayo Aprili 27 nchini Afrika Kusini ambapo mshindi wa jumla atafanikiwa kutinga fainali ya michuano hii.

X1: Camara, Kapombe Zimbwe Jr (Nouma 73′), Chamou (Mavambo 80′), Hamza, Kagoma, Kibu (Mutale 73′) Ngoma, Mukwala (Ateba 84′), Ahoua, Mpanzu

Waliionyeshwa kadi: Nouma 90+3′

X1: Oscarine, Olivier, Enyinnaya (Mchana 58′), Nduli (Phili 79′) De Jong (Barns 70′), Basadien, Thabo, Jabaar (Palace 79′), Devin, Lesiba (Lekoloame 58′), Khiba

Waliionyeshwa kadi: Enyinnaya 35′ Jabaar 36′

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER