Mchezo wetu wa kirafiki wa Kimataifa katika kilele cha Simba Day uliopigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam umemalizika kwa ushindi wa mabao 2-0.
Abdulazak Hamza alitupatia bao la kwanza kwa kichwa dakika ya sita baada ya kumalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Jean Charles Ahoua.
Baada ya kupata hilo tuliendelea kutengeneza nafasi kadhaa lakini hata hivyo hatukuweza kuzitumia vizuri.
Steven Mukwala alitupatia bao la pili dakika ya 48 baada ya kuunganisha mpira wa krosi uliopigwa na Ladaki Chasambi.
Gor Mahia waliongeza kasi baada ya bao la pili na kufika mara kwa mara langoni lakini idara ya ulinzi iliyokuwa chini ya Rushine De Reuck iliweza kuzuia hatari zote.
X1: Camara (Yakoub 31′ Erasto 83′)), Chasambi (Duchu 83′) , Mligo (Abraham 64′), De Reuck, Chamou (Kagoma 45′ Nangu 83′), Hamza (Mzamiru 83′), Kibu (Mpanzu 45′), Naby (Masinde 83′), Sowah (Mukwala 45′ Mwalimu 65′), Ahoua (Kante 83′), Maema (Mutale 65′)
Waliionyeshwa kadi:
X1: Gad, Ochuoga (Bandi 59′), Owino, Kibwage, Morrison (Onyango 53′), Lawrence, Mark (Odhiambo 41′), Bryton, Christopher, Samwel, Ebenezer (Stanley 71′)
Waliionyeshwa kadi: Joshua Onyango 90′