Tumefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC huku tukivunja mwiko katika Uwanja wa Majaliwa kutokana na kutopata alama tatu katika miaka miwili mfululizo iliyopita.
Mlinzi wa kati wa Namungo Derick Mukombozi alionyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja dakika ya 35 baada ya kucheza mchezo usio wa kiungwana.
Jean Charles Ahoua alitupatia bao la kwanza dakika ya 49 kipindi cha kwanza kwa mkwaju wa penati baada ya mlinzi Shomari Kapombe kufanyiwa madhambi ndani ya 18.
Leonel Ateba alikosa mkwaju wa penati uliookolewa na mlinda mlango Jonathan Nahimana dakika ya 51 baada ya Elie Mpanzu kufanyiwa madhambi ndani ya 18 na Hassan Kibailo.
Ahoua alitupatia bao la pili dakika ya 72 kwa mkwaju wa penati baada ya Kapombe kufanyiwa madhambi ndani ya 18 na Anthony Mlingo.
Steven Mukwala alitupatia bao la tatu dakika ya 92 baada ya shuti kali lililopigwa na Valentine Nouma kumgonga mlinzi wa Namungo kabla ya kumkuta mfungaji.
Ushindi huu unatufanya kufikisha pointi 50 tukiwa na nafasi ya pili kwenye msimamo baada ya kucheza mechi 19 huku tukiwa na mchezo mmoja mkononi.
X1: Nahimana, Kibailo, Mlingo, Amoah, Nyoni, Mukombozi, Masawe (Manyanya 85′) Nyenye, Joshua (Ngoy 45′), Najim (Sentawa 90′) Mkola (Abushee 90′)
Walioonyeshwa kadi: Nyoni 27′ Masawe 35 Mukombozi (35 nyekundu) Joshua 45+6′ Amoah 70′
X1: Camara, Kapombe (Duchu 75′), Zimbwe Jr (Nouma 83′), Che Malone, Hamza, Kagoma, Chasambi (Awesu 75′), Ngoma, Ateba (Mukwala 75′), Ahoua (Kibu 83′) Mpanzu
Walioonyeshwa kadi: Awesu 83′