Tumetoshana nguvu na CSKA Moscow

 

Mchezo wetu wa pili wa kirafiki dhidi ya CSKA Moscow ya Urusi uliopigwa katika Mji wa Abu Dhabi umemalizika kwa sare ya mabao 2-2.

CSKA walipata bao la mapema dakika ya nne kupitia kwa mshambuliaji, Fedor Chalov baada ya kuwazidi ujanja walinzi wetu wa kati.

Dakika ya 30 CSKA walipata bao la pili kupitia kwa Jesus Mediana akimalizia mpira wa krosi kutoka upande wa kulia kufuatia walinzi wetu kuzembea kuondoa hatari.

Mabao yetu mawili yalifungwa na Habib Kyombo, ambapo alitupatia bao la kwanza dakika ya 48 baada ya kupokea pasi safi kutoka Saido Ntibazonkiza akiwa katikati ya msitu.

Kyombo tena alitupatia bao la kusawazisha dakika ya 84 baada ya kumalizia pasi iliyopigwa kiufundi na kiungo fundi Clatous Chama.

Kocha Mkuu Roberto Oliviera ‘Robertinho’ aliwatoa Pape Sakho, Erasto Nyoni na Ntibazonkiza na kuwaingiza Habib Kyombo, Mzamiru Yassin na Kibu Denis.

Baada ya mchezo wa leo kambi yetu ya mazoezi Mjini Dubai itakuwa imemalizika na kikosi kitaanza taratibu za safari ya kurejea jijini Dar es Salaam.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER