Mchezo wetu wa hatua ya 16 bora ya CRDB Bank Federation Cup dhidi ya Mashujaa FC uliopigwa Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma umemalizika kwa kupoteza kwa mikwaju ya penati 6-5.
Mchezo huo ambao tulimiliki sehemu kubwa ulimalizika kwa sare ya kufungana bao moja katika muda wa kawaida.
Ralient Lusajo aliipatia Mashujaa bao la uongozi dakika ya tano baada ya kumalizia mpira wa kona uliopigwa na Mpoki Mwakinyuke.
Baada ya bao hilo tuliongeza kasi ya mashambulizi kwa kuliandama lango la Mashujaa lakini hata hivyo walikuwa imara kwenye kuzuia.
Kiungo mkabaji Said Makapu alitolewa kwa kadi nyekundu kufuatia kuonyeshwa ya pili ya njano baada ya kumchezea madhambi Saido Ntibazonkiza.
Freddy Michael alitupatia bao la kusawazisha dakika ya 51 kwa shuti la chini chini baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Kibu Denis.
Penati zetu zilifungwa na Zimbwe Jr, Israel Patrick, Freddy, Mzamiru Yassin
X1: Johola, Rauf, Mwakinyuke, Madereke Mtuwi, Makapu, Mgandila (Dabi 58′), Balama (Ulomi 83′)@, Lusajo Adam, Omary (Idrisa 76′)
Walioonyeshwa kadi: Adam Adam 31′ Makapu 33′ 47′ Johola 90+3
X1: Ally, Israel, Zimbwe Jr, Kennedy, Che Malone, Babacar, Kibu (Mzamiru 83′), Ngoma (Onana 45′), Jobe (Freddy 45′), Ntibazonkiza (Kanoute 64′), Chama (Chasambi 83′)
Walioonyeshwa kadi: