Tumetoka sare na Bunda Queens

Kikosi chetu cha Simba Queens kimetoka sare ya bila kufungana na Bunda Queens katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake uliopigwa katika Uwanja wa Karume Musoma.

Mchezo huo ulikuwa mkali huku tukimiliki sehemu kubwa na kutengeneza nafasi kadhaa za kufunga lakini hatukuweza kuzitumia.

Wenyeji Bunda walikuwa wakifanya mashambulizi ya kushtukiza lakini hata hivyo tulikuwa makini kuhakikisha tunawadhibiti.

Kocha Msaidizi Mussa Hassan Mgosi alifanya mabadiliko ya kuwatoa Danai Bhobho, Jentrix Shikangwa na Asha Djafar na kuwaingiza Dotto Evarist, Ritticia Nabbosa na Mwanahamisi Omary.

Matokeo haya yanatufanya kufikisha pointi 13 tukiendelea kusalia nafasi ya pili.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER