Kikosi chetu kimefanikiwa kutinga robo fainali ya michuano ya CRDB Federation Cup baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Bigman katika mchezo uliopigwa Uwanja wa KMC Complex.
Joshua Mutale alitupatia bao la kwanza dakika ya 15 kwa shuti la mguu wa kushoto akiwa ndani ya 18 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Valentine Nouma.
Leonel Ateba alitupatia bao la pili kwa mkwaju wa penati dakika ya 30 kufuatia Elie Mpanzu kufanyiwa madhambi ndani ya 18.
Joseph Mussa aliwapatia Bigman bao la kwanza dakika ya 45 kwa shuti nje ya 18 baada ya kuwazidi ujanja walinzi wetu.
Kipindi cha pili tulitengeneza nafasi kadhaa za kufunga lakini Bigman walikuwa makini kuhakikisha hawafanyi makosa ambayo yangewagharimu.
X1: Abel, Kijili (Chamou 62′) Duchu, Kazi, Ngoma, Mpanzu (Chasambi 40′), Deborah (Okajepha 81′) Ateba (Mukwala 81′), Ahoua (Awesu 81′), Mutale
Walioonyeshwa kadi: Kazi 45′