Tumetinga Nusu Fainali ya CRDB Federation Cup

Kikosi chetu kimefanikiwa kutinga nusu fainali ya michuano ya CRDB Federation Cup baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mbeya City katika mchezo uliopigwa Uwanja wa KMC Complex.

Tulianza mchezo huo kwa kasi huku tukifika zaidi langoni mwa City ambao muda mwingi walikuwa nyuma huku walifanya mashambulizi machache ya kushtukiza.

Mudathir Said aliipatia Mbeya City bao la kwanza dakika ya 22 kwa shuti kali la mguu wa kushoto lililomshinda mlinda mlango Ally Salim kufuatia walinzi wetu wakati kujichanganya.

Kiungo Fabrice Ngoma alitusawazishia bao hilo dakika ya 24 kwa kichwa baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Ladaki Chasambi.

Leonel Ateba alitupatia bao la pili dakika ya 29 kwa kichwa baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Ngoma.

Joshua Mutale alitupatia bao la tatu dakika ya 43 baada ya kupokea pasi ya Ngoma na kuwapiga chenga walinzi wa City na kupiga shuti la chini chini lililomshinda mlinda mlango Hashim.

Kipindi cha pili kasi ya mchezo ilipungua ingawa tuliendelea kumiliki sehemu kubwa na kutengeneza nafasi kadhaa lakini hatukuweza kuzitumia.

Ushindi huu utatufanya kukutana na mshindi kati ya Singida Black Stars na Kagera Sugar katika mchezo wa nusu fainali.

X1: Ally, Duchu, Nouma, Karaboue (Balua 54′), Hamza (Okajepha 61′), Ngoma (Kapombe 77′) Chasambi, Fernandez, Ateba (Mukwala 77′), Awesu (Adolf 87′) Mutale

Waliionyeshwa kadi:

X1: Hashim, Mwasa, Daniel, Mwalyanzi, Mwaipola, Mwakatundu, Willy (Mussa 78′) Adilly, Chesko, Jeremiah, Mudathir (Riphat 45′)

Waliionyeshwa kadi: Mudathir 49′ Chesco 62′

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER