Kikosi chetu kimefanikiwa kutinga fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kutoka sare ya bila kufungana dhidi ya Stellenbosch katika mchezo wa nusu fainali ya pili uliopigwa Uwanja wa Moses Mabhida jijini Durban.
Tumefanikiwa kutinga fainali kwa jumla ya bao moja kufuatia ushindi wa bao moja tuliopata kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Amaan Zanzibar, Aprili 20.
Mchezo ulianza kwa kasi ya kawaida huku wenyeji Stellenbosch wakifika langoni kwetu mara kadhaa lakini tulikuwa imara kuhakikisha tunaendelea kuwa salama.
Dakika ya 24 Kibu Denis alifanyiwa madhambi ndani ya 18 lakini kupitia msaada wa video za mwamuzi wa akiba (VAR) mwamuzi wa kati alikataa kuweka penati.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku timu zikishambuliana kwa zamu ambapo dakika ya 55 kupitia usaidizi wa VAR mwamuzi alikataa mkwaju wa penati ambapo alidhani Karabou Chamou ameshika ndani ya 18.
X1: Masuluke, Toure, Moloisane, Basadien, Enyinnaya (Nku 69′), Nduli (Philander 82′) Khiba, Butsaka (Palace 63′), De Jong, Titus, Lekoloane (Barns 63′).
Waliionyeshwa kadi: Toure 53′
X1: Camara, Kapombe, Zimbwe Jr(Nouma 85′), Chamou, Hamza, Kagoma, Kibu, Ngoma, Mukwala (Ateba 54′), Ahoua (Fernandez 64′) Mpanzu (Che Malone 85′)
Waliionyeshwa kadi: Camara 85′