Tumefanikiwa kutinga hatua ya 32 bora ya CRDB Federation Cup kwa kishindo baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 6-0 dhidi ya Kilimanjaro Wonders katika mchezo uliopigwa Uwanja wa KMC Complex.
Valentino Mashaka alitupatia bao la kwanza dakika ya kwanza akimalizia mpira wa krosi uliopigwa na Valentine Nouma.
Ladaki Chasambi alitupatia bao la pili dakika ya tatu baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na David Kameta ‘Duchu’.
Patrick Sebastian alijifunga dakika ya 10 na kutupatia bao la tatu katika jitihada za kuokoa shuti lililopigwa na Augustine Okajepha.
Joshua Mutale alitupatia bao la nne dakika ya 20 kufuatia mlinda mlango wa Kilimanjaro kukosea kutoa pasi iliyomkuta nyota huyo raia wa Zambia.
Steven Mukwala alitupatia bao la tano dakika ya 48 kwa kichwa baada ya kumalizia vema mpira wa krosi uliopigwa na Duchu.
Dakika ya 80 Edwin Balua alitupatia bao sita kwa shuti la chini chini akiwa ndani ya 18 lililomshinda mlinda mlango wa Kilimanjaro.
X1: Ally, Duchu, Nouma, Chamou, Hamza (Kijili 82′), Okajepha (Balua 45′), Chasambi, Mzamiru (Fernandez 65′), Mashaka (Mukwala 45′), Awesu (Omary 30′), Mutale