Tumetinga 16 bora CRDB Federation Cup

Kikosi chetu kimefanikiwa kutinga hatua ya 16 bora ya michuano ya CRDB Federation Cup baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya TMA Stars katika mchezo uliopigwa Uwanja wa KMC Complex.

Mlinzi wa kushoto, Valentine Nouma alitupatia bao la kwanza dakika ya 17 kwa mpira wa adhabu uliotinga wavuni moja kwa moja baada ya Awesu Awesu Awesu kufanyiwa madhambi nje ya 18.

Dakika mbili baadae Sixtus Sabilo alijifunga na kutupatia bao la pili katika jitihada za kuokoa mpira wa krosi uliopigwa na Ladaki Chasambi.

Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi ya kawaida huku tukimiliki sehemu kubwa ya mchezo na kufanya mashambulizi mengi langoni mwa TMA lakini tulikosa ufanisi wa kutumia nafasi tulizopata.

Leonel Ateba alitupatia bao la tatu dakika ya 75 kwa kichwa baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Kelvin Kijili.

Ushindi huu unatufanya kukutana na timu ya Big Man inayoshiriki Championship kutoka Korogwe, Tanga kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora baadae mwezi ujao.

X1: Ally, Kapombe, Nouma, Chamou (Kijili 71′) Hamza (Kagoma 45′), Okajepha (Omary 56′) Chasambi, Deborah (Mashaka 77′) Ateba, Mutale, Awesu (Balua 71′)

Waliionyeshwa kadi: Hamza 34′ Kapombe 82′

X1: Ismail, Better, Siraji, Asanga (Mahimbo 45′), Vedastus, Hemed, Paul (Gabriel 61′) Sudi, Sabilo (Malmusi 61′), Kassim, Kapera (Omary 76′)

Waliionyeshwa kadi: Siraji 58′

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER