Klabu yetu leo imeingia mkataba wa ushirikiano na Western Armenia Football Club inayoshiriki Ligi Kuu ya Armenia, Ulaya ya Mashariki.
makubaliano ya ushirkiano huo yatakuwa kwenye maeneo makubwa manne, Kiufundi, Ubadilishanaji na uuzianaji wa wachezaji, Soka la vijana na mafunzo kwa wakufunzi.
Akizungumza kwenye hafla hiyo Rais wa Western Armenia (alievaa shati jeusi) Andrenik Martirosyan amesema anayo furaha kuingia kwenye ushirikiano huu sababu Simba moja ya timu kubwa barani Afrika hivyo anaamini makubaliano haya yatakuwa faida kwa klabu zote.
“Ni furaha kwetu kuingia katika makubaliano haya, Simba ni timu kubwa Afrika na inafanya vizuri tunaamini ushirikiano huu utakuwa na faida kwetu sote,” amesema Adrenik.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Klabu, Imani Kajula amesema ushirikiano huu utatoa fursa kwa wachezaji wetu kwenda kucheza soka Ulaya na wale wa Armenia kuja kwetu.
Kajula ameongeza kuwa uzoefu ambao watapata wakufunzi wetu kutoka Western itakuwa msaada kwa ajili ya kufanya vizuri kwenye michuano ya ndani pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika.
“Simba inayo furaha kushirikiana na western Armenia FC katika maeneo sambayo yatatoa fursa kwa wachezaji wetu kwenda kucheza soka Ulaya, maendeleo ya soka ya vijana pamoja na wakaufunzi wetu kupata uzoefu.
“Simba inaamini kwenye mahusiano na klabu nyingine duniani ikiwa ni njia ya kubadilishana uzoefu na utaalamu na pia kukuza fursa kwa klabu pamoja na wachezaji wake,” amesema Kajula.
Katika hafla ya utiaji huo wa saini Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Salim Abdallah ‘Try Again’ nae amehudhuria.