Kikosi chetu kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Tabora United katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora na kutufanya kurejea kileleni mwa msimamo.
Tulianza mchezo huo kwa kasi huku tukifika mara nyingi langoni mwa Tabora ingawa tulikosa ufanisi wa kumalizia nafasi tulizopata.
Leonel Ateba alitupatia bao la kwanza dakika ya 12 kwa shuti kali nje ya 18 baada ya kupokea pasi safi ya Elie Mpanzu.
Ateba alitupatia bao la pili kwa mkwaju wa penati dakika ya 34 baada ya Mpanzu kufanyiwa madhambi ndani ya 18 na mlinzi wa Tabora.
Kipindi cha pili tuliongeza kasi ya kutafuta mabao zaidi huku Tabora nao wakifika mara kadhaa langoni kwetu lakini tulikuwa imara kuwadhibiti.
Shomari Kapombe alitupatia bao la tatu dakika ya 65 kwa shuti la chini chini la mguu wa kushoto baada ya kumalizia pasi safi iliyopigwa na Ateba.
Ushindi huu umetufanya kufikisha alama 43 tukirejea kileleni mwa msimamo baada ya kucheza mechi 16.
X1: Camara, Kapombe, Zimbwe Jr, (Nouma 71′) Che Malone, Hamza, Kagoma, Kibu (Chasambi 52′) Ngoma (Fernandez 71′), Ateba, (Mukwala 71′), Ahoua, Mpanzu (Mutale 71′)
Walioonyeshwa kadi: