Ushindi wa mabao 3-0 tuliopata dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo uliopigwa Uwanja wa KMC Complex umetufanya kurejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC.
Tulianza mchezo kwa kasi huku tukitafuta bao la mapema dakika 20 za mwanzo tulifanya mashambulizi ya hatari sita langoni mwa Prisons lakini kikwazo kikawa mlinda mlango Sebusebu Samson.
Jean Charles Ahoua alitupatia bao la kwanza dakika ya 29 kwa shuti kali ndani ya 18 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Shomari Kapombe.
Elie Mpanzu alitupatia bao la pili dakika ya 45 kwa shuti kali la chini chini akiwa ndani ya 18 baada ya kupokea pasi ya Leonel Ateba.
Dakika moja baadae Ladaki Chasambi alitupatia bao la tatu baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Kapombe.
Matokeo haya yametufanya kufikisha alama 47 baada ya kucheza michezo 18 na kurejea kileleni.
X1: Camara, Kapombe, Zimbwe Jr (Nouma 64′) Che Malone, Hamza (Chamou 33′) Kagoma (Fernandez 45′) Chasambi (Balua 64′) Ngoma (Mukwala 75′), Ateba, Ahoua, Mpanzu
Walioonyeshwa kadi: Chamou 55′
X1: Sebusebu, Sabiyanka(Mwalugara 85′), Momande, Mwaituka, Ngasa, Sufian, Abraham (Mwasilindi 58′) Mwihambi, Adam (Sengati 81′) Seleman (Sageja 58′), Mhilu
Walioonyeshwa kadi: