Tumepoteza taji la Ubingwa wa Shirikisho Afrika

Mchezo wetu wa fainali ya mkondo wa pili wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS Berkane umemalizika kwa sare ya kufungana bao moja hivyo tumeshindwa kutwaa ubingwa wa michuano hii

Joshua Mutale alitupatia bao la kwanza dakika ya 17 kwa mguu wa kushoto akiwa ndani ya 18 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Elie Mpanzu.

Dakika ya 22 Shomari Kapombe alipoteza nafasi ya wazi baada ya mpira wa kichwa aliopiga kupaa juu ya lango kufuatia krosi safi iliyopigwa na Mutale.

Kiungo wa kati Yusuph Kagoma alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano dakika ya 50 baada ya kumfanyia madhambi mchezaji wa Berkane.

Steve Mukwala alitupatia bao la pili kwa kichwa dakika ya 74 baada ya kumalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Jean Charles Ahoua.

Ismail Sibibe aliisawazishia Berkane bao hilo dakika ya nne ya nyongeza kipindi cha pili baada ya kumzidi ujanja mlinzi Valentine Nouma.

Berkane wametwaa ubingwa huo kwa jumla ya mabao 3-1 kufuatia ushindi wa 2-0 waliopata nyumbani wiki iliyopita.

X1: Camara, Kapombe, Zimbwe Jr (Nouma 82′) Chamou, Che Malone (Ateba 83′), Kagoma, Mutale (Kibu 70′) Ngoma, Mukwala, Ahoua, Mpanzu

Waliionyeshwa kadi: Kagoma 35′ 50′ (Nyekundu)

X1: Munir, Dayo, Tahif, Elmoussoui, Assal, Camara (Sidibe 77′), Lebhiri, Khairi (El Morabit 68′), Mehri, Riahi (Bassene 59′) Lamlioui (Zghoudi 77′)

Waliionyeshwa kadi: Khairi 41′ Riahi 59′ Camara 72′

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER