Tumepoteza pointi tatu ugenini

Kikosi chetu kimepoteza pointi tatu muhimu ugenini baada ya kufungwa mabao 2-0 dhidi ya RS Berkane katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika uliofanyika Uwanja wa Manispaa ya Berkane nchini Morocco.

Tulianza mchezo huo kwa kasi ya chini huku tukiwaachia utawala wenyeji Berkane na kufanya mashambulizi machache.

Wenyeji Berkane walipata bao la kwanza dakika ya 31 kupitia kwa Adama Ba baada ya kupiga mpira wa adhabu uliotinga wavuni moja kwa moja.

Dakika ya 40 Berkane walipata bao la pili kupitia kwa El Bahri kwa kichwa akimalizia mpira wa kona huku walinzi wetu wakiruhusu aruke hewani akiwa huru.

Kipindi cha pili tuliongeza kasi katika ushambuliaji hasa baada ya kuingia Bernard Morrison lakini hata hivyo hatukuweza kuzitumia nafasi hizo ipasavyo.

Kocha Mkuu Pablo Franco aliwatoa Peter Banda, Sadio Kanoute na Pape Sakho na kuwaingiza Morrison, Jimmyson Mwanuke na Yusuf Mhilu.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER