Mchezo wetu wa pili wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca kutoka Morocco uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa umemalizika kwa kupoteza mabao 3-0.
Tulianza mchezo kwa kasi kutafuta bao la mapema lakini Raja walikuwa makini huku wao wakifanya mashambulizi ya kujibu kila tunapopoteza mpira.
Hamza Khabba aliwapatia Raja bao la kwanza dakika ya 30 kwa shuti kali nje kidogo ya 18 baada ya kugongeana pasi kutoka katikati ya uwanja.
Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi tukimiliki mpira zaidi lakini Raja waliziba mianya yote huku wao wakiendelea kufanya mashambulizi yakujibu.
Sofiane Benjdida aliwapatia Raja bao la pili dakika ya 83 baada ya kumalizia pasi safi kutoka kwa Bentayg.
Dakika mbili baadae mlinzi wa kati wa Raja Ismail Mukadem aliwapatia bao la tatu kwa mkwaju wa penati baada ya mlinzi Joash Onyango kucheza madhambi ndani ya 18.
X1: Manula, Kapombe, Zimbwe Jr, Onyango, Inonga, Sawadogo (Mkude 45), Sakho (Phiri 73), Mzamiru, Bocco (Baleke 58), Saido, Chama.
Walionyeshwa kadi: Ntibazonkiza 90+3′.
X1: Zniti, Mukadem, Harkass, Badaoui, Bentayg, Aholoui, Makahasi (Hafidi 88), Zrida (Sabbar 70), Bouzok, Habti (Benguit 75) Khabba (Benjdida 75)
Walionyeshwa kadi: Bouzok 39′ Zniti 73′.
One Response
Huyo sanko na sawadogo aisee dah wambie waache utoto