Kikosi chetu kimeanza Michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa kupoteza baada ya kufungwa bao moja dhidi ya Mlandege katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Amani.
Mchezo ulianza kwa kasi tukishambuliana kwa zamu huku tulifika zaidi langoni kwao lakini tulikosa umakini wa kutumia nafasi tulizotengeneza.
Mlandege wao walifanya mashambulizi machache ya kushtukiza lakini hata wao walikosa umakini kwenye eneo la mwisho la kumalizia.
Bao pekee la mchezo huo limefungwa na kiungo Aboubakar Mwadini kwa kichwa dakika ya 75 akimalizia mpira wa kona.
Kocha Juma Mgunda alifanya mabadiliko ya kuwatoa Nelson Okwa, Michael Joseph na Kibu Denis na kuwaingiza Victor Akpan, Joseph Mbaga na Hassan Mussa.