Mchezo wetu wa Ngao ya Jamii wa kuashiria kufunguliwa kwa msimu huu wa mashindano 2025/2026 dhidi ya watani wa jadi Yanga uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa umemalizika kwa kupoteza kwa bao moja.
Mchezo ulianza kwa kasi ya kawaida huku timu zikicheza kwa mipango lakini tulifika zaidi langoni mwa Yanga na kutengeneza nafasi ambazo hatukuzitumia vizuri.
Mlinzi wa kati, Abdulazak Hamza alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kuumia mguu kufuatia kugongana na Mudathir Yahya dakika ya 24.
Pacome Zouzoua aliipatia Yanga bao hilo dakika ya 54 kufuatia shuti lililopigwa na Maxi Nzengeli kuzuiliwa na mlinda mlango Moussa Camara.
Baada ya bao hilo tuliendelea kutengeneza nafasi na kushambulia lakini tulikosa ufanisi wa kuzitumia.
X1: Diara, Mwenda, Boka (Zimbwe Jr’ 65′), Bacca, Job, Abuya (Conte 75′), Nzengeli (Ecua 75′) Andambwile, Dube (Mzize 57′), Mudathir (Doumbia 45′), Pacome,
Waliionyeshwa kadi: Boka 32′ Diara 82′ Andambwile 90+10′
X1: Camara, Kapombe, Naby, De Reuck, Hamza (Karaboue 24′), Kagoma, Kibu, Kante (Mligo 59′), Mukwala (Mwalimu 73′), Ahoua, Mpanzu (Maema 73′)
Waliionyeshwa kadi: Kante 53′ Camara 54′ Kapombe 56′ Kagoma 60′ Naby 90+8′