Tumepoteza mchezo wa mkondo wa kwanza wa Robo Fainali

Kikosi chetu kimepoteza mchezo wa mkondo wa kwanza wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kufungwa mabao 2-0 na Al Masry katika mtanange uliopigwa Uwanja wa Suez Canal.

Abderahim Deghmoum aliwapatia Al Masry bao la kwanza dakika ya 15 kwa shuti kali la mguu wa kushoto nje ya 18 lililomshinda mlinda mlango, Moussa Camara.

Baada ya bao hilo tuliongeza utulivu na kucheza kwa ungalifu huku tukihakikisha tunawanyima nafasi ili wasiweze kutudhuru huku tulitengeneza nafasi kadhaa.

Kipindi cha pili tuliongeza kasi huku tulifikia zaidi ya lango la Al Masry ingawa walikuwa imara kuhakikisha hawaruhusu bao.

John Okoye aliwapatia Al Masry bao la pili dakika ya 90 akimalizia mpira wa krosi uliopigwa kutoka upande wa kushoto wa uwanja ambao walinzi wetu walishindwa kuukoa.

Mchezo wa mkondo wa pili utapigwa Jumatano ijayo katika Uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo mshindi wa jumla atatinga nusu fainali.

X1: Camara, Kapombe, Zimbwe Jr, Chamou, Hamza, Kagoma, Kibu, Ngoma, Ateba (Mukwala 78′), Ahoua, Mpanzu

Waliionyeshwa kadi: Chamou 87′

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER