Kikosi chetu kimepoteza mechi ya kwanza katika msimu huu wa Ligi Kuu ya NBC kwa bao moja dhidi ya Mbeya City uliopigwa katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Paul Nonga aliwafungia City bao hilo dakika ya 19 baada ya kuwazidi ujanja walinzi wetu kufuatia mpira mrefu uliopigwa na Juma Shemvuni na kugongwa kichwa na Frank Ikobela.
Dakika 15 za mwisho kuelekea mapumziko tuliongeza kasi kwa kuliandama lango la City na kufanya mashambulizi ambayo hatuku ya tumia vizuri.
Nahodha wa City, Mpoki Mwakinyuke alitolewa nje ya uwanja baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano kwa kumfanyia madhambi Chris Mugalu.
Dakika ya 47 Mugalu alikosa mkwaju wa penati baada ya mlinzi wa City kuunawa mpira katika harakati za kuokoa krosi ya Kibu.
Kocha Pablo Franco aliwatoa Mzamiru Yassin, Kibu, Jonas Mkude, Mohamed Hussein na Henock Inonga na kuwaingiza John Bocco, Pape Sakho, Medie Kagere, Hassan Dilunga na Jimmyson Mwinuke.
3 Responses
Nimeipenda
Tuendelee kupambana.Inahitajika utulivu safu ya ufungaji.