Kikosi chetu kimefanikiwa kupata ushindi wa bao moja katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya JKT Tanzania uliopigwa katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo.
Mchezo ulianza kwa kasi huku tukishambuliana kwa zamu lakini tukifika zaidi langoni mwa JKT ingawa nafasi tulizopata ndani ya dakika 45 za mwanzo tulishindwa kuzibadili kuwa mabao.
Fabrice Ngoma alitupatia bao la kwanza dakika za nyongeza kipindi cha kwanza baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Steven Mukwala.
Kipindi cha pili tuliongeza kasi na kutengeneza nafasi lakini umakini wa kuzitumia ulikuwa mdogo.
Ushindi huu unatufanya kufikisha alama 63
baada ya kucheza mechi 24.
X1: Camara, Kapombe, Nouma (Zimbwe Jr 85′), Kagoma, Hamza, Ngoma, Kibu, Fernandez (Che Malone 68′), Mukwala (Mpanzu 55′), Ahoua, Mutale (Ateba 84′),
Waliionyeshwa kadi: Ngoma 88″
X1: Yakoub, Salum, Karim, Katanga, Msengi, Bausi (Ndemla 54′), Maka, Nassor (Songo 67′) Najim (Dilunga 45′), Mudy, Kuchuya
Waliionyeshwa kadi: Nassor 03′ Bausi 21′ Kichuya 40′ Mousy 45′