Tumepata ushindi dhidi ya Dar City

Kikosi chetu kimefanikiwa kupata ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Dar City katika mchezo wa kirafiki uliopigwa Uwanja wa Mo Simba Arena.

Mchezo wa leo ni wa kwanza kwa mlinda mlango Aishi Manula tangu alivyopata majeraha yaliyomuweka nje ya uwanja kwa miezi minne.

Tulianza mchezo huo kwa kasi huku tukiliandama la lango ya Dar City ambao walikuwa walizuia muda mrefu na kutupa nafasi ya kumiliki mpira.

Tulifanikiwa kupata mabao manne kipindi cha kwanza kupitia kwa Shabani Chilunda kwa mkwaku wa penati dakika ya tano, Willy Onana aliongeza la pili dakika ya 12 huku Chilunda akiongeza la tatu dakika ya 19 na Luis Miquissone akitupia dakika ya 24.

Dar City walirudi kwa kasi kipindi cha pili na waliongeza nguvu kwenye lango letu ambapo walifanikiwa kupata bao la kufutia machozi dakika ya 51.

Said Ntibazonkiza alikamilisha karamu ya mabao kwa kufunga la bao la mwisho kwa mkwaju wa penati dakika ya 84.

Kikosi Kamili kilichopangwa:

Manula (Abel 40′), Duchu (Kapombe 71′), Jimmyson (Zimbwe Jr’ 71′), Kennedy (Kapama 45′), Kazi (Che Malone 71′), Abdallah (Ngoma 71′), Luis (Ntibazonkiza 71′), Kanoute, Chilunda (Baleke 45′) (Mody 71), Phiri, Onana (Jimmyson 84′).

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER