Tumepata pointi moja Ivory Coast

Mchezo wetu wa hatua ya makundi ya Ligi Kuu ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASEC Mimosas uliopigwa Uwanja wa Felix – Houphouet – Boigny umemalizika kwa sare ya bila kufungana.

Mchezo ulianza kwa kasi ya kawaida huku timu zote zikishambuliana kwa zamu huku mpira ukichezwa zaidi katikati ya uwanja.

Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi kwa kuliandama lango la ASEC ambapo dakika ya 46 Sadio Kanoute alipoteza nafasi ya wazi baada ya kumzidi ujanja mlinda mlango lakini shuti lake lilitoka pembeni kidogo.

Tuliendelea kutengeneza nafasi huku wenyeji ASEC nao wakija golini kwetu mara kadhaa lakini hakuna aliyeweza kutumia nafasi zilizopatikana.

Matokeo haya yanatufanya kuendelea kubaki nafasi ya pili tukiwa na pointi sista baada ya kucheza mechi tano.

X1: Folly, Wonlo, Ande, Mofosse, Diarrassouba, Bada, Tra Bi, Aka, Poku (Kone 90′) Avo (Berthe 69′), Zouzoua

Walioonyeshwa kadi: Ande 48′

X1: Manula, Kapombe, Zimbwe Jr, Che Malone, Henock, Babacar, Ntibazonkiza (Mzamiru 83′) Kanoute (Kibu 68′), Jobe (Kouablan 68′), Ngoma, Chama (Miqussone 83′)

Walioonyeshwa kadi: Kanoute 21′ Jobe 24′ Kouablan 78′

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER