Maelfu ya mashabiki wamejitokeza kwa wingi kukipokea kikosi chetu baada ya kuwasili jijini Mbeya kwa tayari kwa mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Tanzania Prisons.
Tangu tulivyoshuka Uwanja wa Ndege tumewakuta mashabiki wengi wakitusubiri kwa ajili ya kuwalaki wachezaji.
Mashabiki wetu wa Mbeya wametufanya kujiona tuna deni kubwa na tumejipanga kuhakikisha tunawalipa furaha kwa kupata ushindi kwenye mchezo wa kesho.
Mashabiki wetu kote nchini wameonyesha kuwa pamoja nasi katika nyakati zote nasi tunathamini mchango wao.