Tumefanikiwa kupata alama tatu muhimu baada ya kuibuka na ushindi wa bao moja dhidi ya CS Sfaxien katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika uliopigwa Uwanja wa Hammadi Agrebi nchini Tunisia.
Wenyeji Sfaxien walianza kwa kasi dakika 20 za mwanzo kwa kufanya mashambulizi ya haraka lakini tulikuwa imara kuwadhibiti.
Jean Charles Ahoua alitupatia bao hilo pekee dakika ya 34 kwa shuti kali akiwa ndani ya 18 baada ya kumalizia pasi ya Leonel Ateba kufuatia mpira mrefu uliopigwa na Che Fondoh Malone.
Kipindi cha pili tuliongeza kasi ya kutafuta bao la pili huku tukiwa makini zaidi kwenye kuzuia ili tusiruhusu bao.
Ushindi wa leo umetufanya kufikisha alama tisa na kuwa vinara wa kundi baada ya kucheza mechi nne.
X1: Dahmen, Baccar, Traore (Willy 58′), Harabi, Layouni, Conte, Zaidi (Hmid 58′) Sekkouhi, Becha (Ben Ali 81′), Cristo (Habbesi 68′), Haj Hsan (Habboub 81′)
Walioonyeshwa kadi: Hmid 61′
X1: Camara, Kapombe Zimbwe Jr, Che Malone, Hamza, Kagoma, Kibu (Chamou 86′), Ngoma, Ateba (Mukwala 90′), Mpanzu (Fernandez 76′), Ahoua
Walioonyeshwa kadi: Mpanzu 28′ Ateba 45′