Tumepangwa na Waydad Robo Fainali Ligi ya Mabingwa

Droo ya upangaji wa hatua ya Robo Fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika imekamilika na tumepangwa na Waydad Casablanca kutoka Morocco.

Droo hii inamaanisha tutarudi tena katika jiji la Casablanca kwa mara pili safari hii tunaenda kukutana na Wydad na sio Raja ambao tulikuwanao kundi moja.

Wydad ndio Mabingwa watetezi wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na mchezo wetu wa ugenini utapigwa katika uwanja ule ule wa Mohamed wa tano ambao tulicheza dhidi ya Raja wiki iliyopita.

Mechi za mkondo wa kwanza zitapigwa kati ya Aprili 21-22 wakati zile za marudiano zitapigwa Aprili 28-29.

Sisi tutanzia nyumbani kutokana na kumaliza nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi letu.

Endapo tutafanikiwa kumtoa Wydad tutakutana na mshindi kati ya CR Belouzidad ya Algeria dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini katika hatua ya nusu fainali.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER