Tumepangwa na TMA hatua ya 32 CRDB Federation Cup

Droo ya hatua ya 32 imekamilika mchana huu na tayari tumemjua mpinzani tuliyepangwa nae ambaye ni TMA kutoka Arusha inayoshiriki Ligi Daraja la kwanza (Championship).

Katika mchezo huo sisi ndio wenyeji mechi yenyewe itapigwa kati ya Machi 10-12 katika Uwanja wa KMC Complex.

Mshindi wa mchezo huo atakutana na mshindi kati ya Tanzania Prisons na Big Man katika hatua ya 16 bora.

Mchezo wa hatua ya 16 bora utachezwa kati ya Aprili 1-4.

Tumepata tiketi ya kucheza hatua ya 16 bora baada ya kuifunga Kilimanjaro Wonders mabao 6-0 kwenye mechi ya hatua ya 64 bora iliyopigwa Uwanja wa KMC Complex, Januari 26.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER