Droo ya robo fainali ya michuano ya CRDB BANK federation cup imekamilika na tumepangwa na Mbeya City kutoka Mbeya inayoshiriki Ligi Daraja la kwanza (Championship)
Katika mchezo huo sisi ndio wenyeji mechi yenyewe itapigwa kati ya Aprili 11-13 katika Uwanja wa KMC Complex.
Mshindi wa mchezo huo atakutana na mshindi kati ya Singida Black Star na Kagera Sugar katika nusu fainali.
Mchezo wa nusu fainali utachezwa kati ya Aprili 25-27.
Tumepata tiketi ya kucheza hatua ya robo fainali baada ya kuifunga Bigman FC 2-1 kwenye mechi ya hatua ya 16 bora iliyopigwa Uwanja wa KMC Complex, Machi 27.