Tumepangwa na Ihefu Robo Fainali ya ASFC

Droo ya Robo Fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup imekamilika na tumepangwa na Ihefu FC.

Kwa mujibu wa droo hiyo iliyofanyika leo Machi 15 katika mchezo huo sisi tutakuwa wenyeji.

Mshindi kati yetu atakutana na mshindi kati ya Azam FC dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Nusu fainali utakaopigwa Uwanja wa Nangwanda Sijaona Mkoani Mtwara.

Taji la ASFC tulilipoteza msimu uliopita na moja ya malengo yetu ni kuhakikisha tunalirejesha hivyo tutaweka nguvu katika mchezo dhidi ya Ihefu ili tufuzu nusu fainali.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER