Droo ya hatua ya robo fainali imekamilika Doha, Qatar na tumepangwa kucheza na Al Masry kutoka Misri.
Tutaanzia ugenini mchezo wa kwanza utapigwa kati ya Aprili 1-2 huku mechi ya marudiano ikipigwa kati ya Aprili 8-9.
Tumewahi kukutana na Al Masry kwenye michuano hii ambapo tulipokutana mwaka 2018.
Katika mchezo wa mkondo wa kwanza tukiwa nyumbani tulitoka sare ya mabao 2-2 na mechi ya marudiano nchini Misri ikamalizika kwa sare ya bila kufungana.